Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi Dk Samia Suluhu Hassan, amewataka wajumbe wa Mkutano Mkuu wa chama hicho, kuzingatia katiba, sheria, kanuni na taratibu ili kuwa mfano wa kuigwa na vyama vingine katika uchaguzi wa viongozi wa chama hicho.
Akiongea wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 10 wa chama hicho jijini Dodoma, Rais Dk. Samia amesema wote waliohusika kukoroga uchaguzi ngazi za chini za chama hicho, wemeshughulikiwa na hatua kuchukuliwa.
Rais.Dk Samia amesema CCM, inasisitiza umoja maendeleo na mshikamano wa taifa na ni wajibu wa kila mwanachama ku kutafuta ushindi wa chama katika chaguzi zijazo za serikali za mitaa ana uchaguzi mkuu .
Katika mkutano huo pia amependekeza marekebisho madogo ya katiba ya CCM, kuongeza idadi ya wajumbe wa halamshauri kuu bara na visiwani kutoka 15 hadi 20 kwa kila upande, na wajumbe wa kuteuliwa kutoka saba hadi kumi.
Mkutano Mkuu wa CCM unatarajiwa kuchagua Mwenyekiti wa Taifa na Makamu wake wawili pamoja na wajumbe wa halmashauri kuu ya chama hicho.