Back to top

Wakamba waishio Holili wataka kutambuliwa kama watanzania

06 September 2018
Share

Wananchi wa vijiji vya Mandara na Kibanda Hasara wilaya ya Rombo wanaoishi mpakani mwa Kenya na Tanzania Ushoroba wa Holili wamebainika kuwa raia wa Kenya kabila la Wakamba  ambao wanaitaka serikali kuwatambua kama raia halali wa Tanzania.

Wananchi hao wamebainika baada ya kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Kilimanjaro ikiongozwa na mkuu wa mkoa Bi Anna Mgwira walipotembelea vijiji  hivyo na kukutana na wananchi hao ambao wanasema  wanaishi maeneo hayo kwa muda mrefu bila matatizo.

Wamesema tangu miaka ya 1950 wanaishi katika maeneo hayo na kufanya shughuli zao za kujipatia kipatao katika nchi hizo mbili Kenya na Tanzania kwa uhuru kama raia wa Tanzania.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Rombo Bi. Agness Hokororo amesema  maeneo hayo  yanayokaliwa na wananchi hao hao yanaongoza kwa biashara za magendo na madawa ya kulevya.

Baada kutembelea eneo hilo mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Bi.Anna Mghwira amewataka viongozi wa wilaya ya Rombo kuwa makini wakati wa zoezi la upigaji kura pamoja  uandikishaji wa vitambulisho vya uraia  ambavyo wamebainika kuzuiwa hadi hapo muafaka wa uraia wao utakapokamilika.