Back to top

Wananchi Litembo Mbinga waomba kukamilishiwa zahanati yao

31 July 2019
Share

Wananchi wa kijiji cha Litembo katika halmashauri ya wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma, wameiomba serikali kuwasaidia kukamilisha ujenzi wa zahanati yao ili kuwaondolea adha kubwa ya kufuata huduma za matibabu umbali mrefu na kwamba tangu wafanikiwe kuinua kuta kwa nguvu zao na kuezeka bati mwaka jana hadi leo hakuna kinachoendelea.
 
Wananchi hao wa kijiji cha Litembo Mbinga mkoani Ruvuma chenye wakazi zaidi ya 2,800, wametoa ombi hilo la kukamilishiwa ujenzi wa zahanati yao ili ianze kutoa huduma kutokana na adha kubwa wanazopata kufuata matibabu umbali mrefu na kwamba hiyo imekuwa ikihatarisha usalama wa maisha yao hususani akina mama wajawazito.

Hata hivyo mbunge wa jimbo la Mbinga vijijini, Mhe.Martin Msuha aliyetembelea kukagua zahanati hiyo amesema hawezi kuacha nguvu za wananchi zikapotea bure na kuahidi kukamilisha ujenzi wa zahanti hiyo na kuanza kutoa huduma kwa wananchi haraka iwezekanavyo.