Wananchi mkoani Ruvuma wamelalamikia tabia ya madereva wasio waaminifu kumwaga makaa ya mawe pembezoni mwa barabara ili kupakia mizigo mingine na kuomba tabia hiyo idhibitiwe ili kulinda afya za binadamu kwa kuwa makaa hayo yanaingia kwenye mito.
Wameiomba serikali kudhibiti haraka tabia hiyo na kuweka utaratibu wa kuyaondoa makaa yaliyomwagika kandoni mwa barabara baada ya malori ya kubeba makaa ya mawe kupata ajali
Mhandisi migodi wa mkoa wa Ruvuma mhandisi Geti Masawe amesema wana mpango wa kushirikiana na wakala wa barabara TANROADS mkoa wa Ruvuma kupitia mizani na jeshi la polisi ili kudhibiti changamoto hiyo aliyokiri kuwa inawaumiza vichwa
Afisa madini mkaazi wa mkoa wa ruvuma Bw.Jumanne Mohamed amesema kimsingi makaa ya mawe yana athari kwa mimea na binadamu na kuwaonya madereva wanaoyapunguzia kando ya barabara ili kuweka mizigo ya mahindi na viazi kuwa watachukuliwa hatua