Back to top

Wananchi wa Jimbo la Muhambwe washiriki katika zoezi la upigaji kura.

16 May 2021
Share

Wananchi wa Jimbo la Muhambwe wilayani Kibondo mkoani Kigoma wameendelea kushiriki katika zoezi la uchaguzi mdogo huku idadi ndogo ya wapiga kura ikionekana kujitokeza kupiga kura katika vituo mbalimbali. 
.
Wakizungumza na ITV Baadhi ya wapiga kura waliojitokeza wamesema wanaamini uchaguzi utakwenda vizuri na watapata mwakilishi atakayesaidiana nao katika kuleta maendeleo katika jimbo hilo.

Dkt.Florence Samizi - Mgombea Ubunge Jimbo la Muhambwe kupitia CCM


Aidha, Wagombea wa Ubunge katika Jimbo hilo kupitia vyama vya ACT Wazalendo Bw.Julius Masabo na CCM Dkt.Florence Samizi wamesema wameridhishwa na mwenendo wa uchaguzi huo.

Bw.Julius Masabo - Mgombea Ubunge Jimbo la Muhambwe kupitia ACT Wazalendo


Kwa upande wake msimamizi wa uchaguzi katika Jimbo la Muhambwe Ndg.Diocles Lutema amesema zaidi ya wapiga kura laki moja na elfu ishirini na saba wanatarajiwa kupiga kura katika vituo 336 na kwamba hakuna tatizo ambalo limejitokeza katika zoezi la uchaguzi.