Baadhi ya wananchi wameomba Serikali kumuenzi aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Pombe Magufuli kwa kujenga mnara wa sanamu yake ili kuwa kumbukumbu kwa vizazi vilivyopo na vijavyo.
Baadhi ya wananchi wamesema mnara huo utakuwa ni kumbukizi kwa vizazi vya sasa na vijavyo kutokana na mambo aliyolifanyia taifa la Tanzania, ikiwemo kuhamisha makao makuu ya serikali kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma pamoja na ujenzi wa miradi mikubwa ya kimkakati.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji katika Mji wa Chato, Mhandisi Mali Misango amesema ameguswa na kifo cha Dk.John Pombe Magufuli.