Back to top

Wananchi wavamia eneo la TANESCO na kuanza kuchimba madini Morogoro.

14 August 2021
Share

Wananchi wa mtaa wa Mindu kata ya Mindu katika manispaa ya Morogoro wamevamia eneo la Hifadhi la Shirika la Umeme nchini (TANESCO) ambalo linapitisha umeme wa Gridi ya Taifa na kufanya shughuli za uchimbaji wa madini ya dhahabu hali inayohatarisha maisha yao  na miundombinu ya shirika la umeme.

Mhandisi wa Usafirishaji Umeme mkoa wa Morogoro Eng. Amani Abdalah amesema mbali na elimu ya mara kwa mara ambayo wamekuwa wakiwapatia wananchi juu ya kutofanya shughuli kwenye njia hizo, bado baadhi  ya watu wameendelea kukiuka na kuhatarisha usalama wao.