Watu 48 wameripotiwa kupoteza maisha kutokana na mafuriko yaliyobabishwa na mvua zinazoendelea kunyesha nchini Kenya .
Msemaji wa serikali Kanali mstaafu Cyrus Oguna amesema zaidi ya mifugo elfu 17,550 imesombwa na maji huku watu zaidi ya elfu 65 wakikosa makazi.
Serikali ya Kenya imesema shirika la Red cross linafanya jitihada i za kusambaza chakula kwa waathirika wa mafuriko hayo na kwamba raia atakayepoteza maisha kwa kukosa chakula.
Kuhusiana na Mitihani ya Taifa ya shule za Upili ya kidato cha nne KCSE inayoendelea serikali imebainisha kuwa wanatumia helikopta kusambaza mitihani katika maeneo yaliyokumbwa na mafuriko.