Back to top

Waziri Mkuu aagiza kanuni za uendeshaji wa masoko ya madini zikamilike

26 January 2019
Share

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameuagiza uongozi wa wizara ya madini uhakikishe kanuni za uendeshaji wa masoko ya madini katika mikoa yote nchini zinakamilika na kuanza kutumika kwa wakati.

Ameyasema hayo wakati akifungua mkutano kuhusu uanzishwaji wa masoko ya madini katika mikoa yote nchini uliofanyika  jijini Dodoma.

Waziri Mkuu amesema katika kuanzishwa kwa masoko hayo, rasimu ya kanuni imeandaliwa na hivyo ni vema wakazielewa vizuri kwa sababu wao ndiyo watakaozitekeleza kwenye maeneo yao ili Serikali iweze kufikia lengo ililojiwekea katika kuimarisha sekta ya madini.