Back to top

WAZIRI MKUU INDIA ATAKA SULUHISHO UKRAINE DHIDI YA URUSI

23 October 2024
Share

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi, ametolea mwito wa kupatikana kwa suluhisho la vita vya Urusi na Ukraine, Modi ameyasema hayo katika mkutano wa kilele wa kundi la nchi zinazoinukia kiuchumi, (BRICS) huko Kazan, Urusi.

Modi amesema wanaamini kwamba matatizo yanapaswa kutatuliwa kwa amani, na wao wanaunga mkono kikamilifu uanzishwaji wa haraka wa amani na utulivu.

Amesema katika juhudi zao zote wanatoa kipaumbele kwa ubinadamu na wako tayari kutoa msaada wowote unaowezekana katika siku zijazo."

Viongozi wengine wakuu wa nchi na serikali wamesafiri kwenda Urusi kushiriki mkutano huo.

Kwa upande mwingine, Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesema anaitazama Urusi kama "mshirika wa thamani" na rafiki wakati wa mazungumzo na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin.