Ripoti ya Shirika la Afya Duniani (WHO) imeonyesha kuwa idadi ya maambukizi ya magonjwa ya zinaa, kote duniani imeongezeka.
.
Ripoti hiyo iliyotoka Jumanne ya Mei 21, 2024, imeonyesha kuwa watu zaidi ya milioni 1, wenye umri wa kati ya miaka 15 hadi 49, huambukizwa magonjwa ya zinaa kama klamidia, kisonono, kaswende kila siku, huku visa vya kaswende vikionekana kuongezeka kwa kasi zaidi.
.
Ripoti hiyo, pia imeonyesha kuwa kuna ongezeko la kaswende ya kuzaliwa, ambayo hutokea pale ambapo Mama mjamzito anamuambukiza mtoto akiwa tumboni. #via #abcnews