
Yai lenye viini pacha (Double York Egg)
Yai lenye viini pacha kitaalamu kama Double York Egg. Ni yai moja ambalo ukilipasua ndani yake unakuta viini viwili. Mara nyingi mayai haya huwa yana umbo kubwa kuliko mayai yenye kiini kimoja.
.
Yai lenye viini pacha hutokea pale kuku anapotengeneza yai mwilini mwake, Na kuruhusu viini viwili kuingia kwenye gamba moja (single egg shell).
.
Hali hii huwapata zaidi kuku wanaoanza kutaga kwani wanakuwa hawajazoea mzunguko wa kutengeneza mayai ndani ya miili yao. Pia huwapata kuku wanaokaribia kumaliza kutaga.
.
Hakuna aina maalumu ya kuku wanaotaga Yai hili lenye viini viwili lakini yanaweza kutagwa zaidi na aina za kuku ambao ni watagaji wazuri kama Leghorns, Sussex na Rhode Island Red.