Baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya Handeni mkoani Tanga leo limewafukuza kazi zaidi ya watumishi arobaini kwa makosa mbalimbali yakiwemo ya matumizi mabaya ya fedha za halmashauri.
Kwa upande wake afisa utumishi wa halmashauri hii Bi. Fatuma Kalovya amesema kuwa karibia idara zote za halmashauri hii zimeguswa na janga hili.
Naye Afisa utumishi wa halmashauri hiyo amewasihi wale waliosalia kuwa na nidhamu ya kazi ili wasije kumbwa na walioyapata wenzao.