Back to top

Zao la Soya kuwakomboa kiuchumi wakulima Iringa.

08 May 2018
Share

Wakulima zaidi ya 2,000 wa vijiji 9 katika halmashauri ya wilaya ya Iringa wataanza kunufaika na kilimo cha zao la Soya na uhakika wa kuuza zao hilo kwenye masoko 7 yanayonunua zao hilo.

Kupitia mradi wa kukua ni kujifunza wakulima hao wanajengewa uwezo na utaalamu wa kuzalisha kwa wingi zao hilo ili kunufaika zaidi kiuchumi.

Akizungumza na Wakulima hao Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Iringa Bwana Robert Masunya amewahimizi wananchi kuzalisha kwa bidii zao hilo mbadala la biashara ambalo litawakomboa kiuchumi na kuwaondoa katika hali ya umasikini.

Naye Afisa Kilimo wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa Bi.Lucy Nyalu amesema uzalishaji wa zao la Soya kwa wakulima wa wilaya hiyo upo chini licha ya zao hilo kuwa na soko la uhakika.