Back to top

AHUKUMIWA MIAKA 20 JELA KISA SHAMBULIO LA AIBU

29 February 2024
Share

Mahakama ya Wilaya ya Bukoba, imemuhukumu Munziru Mudrikati (19), Mkazi wa Mtaa wa Nyakanyasi uliopo Manispaa ya Bukoba, mkoani Kagera, kwenda jela miaka 20, baada ya kumtia hatiani kwa kosa la shambulio la aibu la kumchezea sehemu za siri kwa uume wake mtoto wa kike (9), ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tatu.
.
Mudrikati, alitenda kosa hilo Agosti 11, 2023, majira ya saa tatu na nusu Asubuhi, huko katika mtaa wa Nyakanyasi, Manispaa ya Bukoba, mkoani Kagera, baada ya kumrubuni mtoto huyo kuwa anaenda kumpa papai na pipi na kumuingiza chumbani kisha kuanza kumsugua na uume wake sehemu ya juu ya ukeni mwa mtoto huyo.
.
Mshitakiwa huyo amehukumiwa kifungo hicho ili iwe fundisho kwa wahalifu wanao jihusisha na vitendo vya ukiukaji wa sheria, maadili na ukatili dhidi ya watoto.