Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimetoa msimamo wake juu ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu, ambapo kimeeleza kuwa maoni ya baadhi ya watu, juu ya kuondolewa kwa mikopo hiyo hayatazingatiwa kwani hakuna haja ya kumpangia matumizi ya fedha mtu mzima.
.
Msimamo huo umetolewa ikiwa ni siku chache tangu Mbunge wa Bunda Vijijini, Peter Getere, akiwa bungeni kuomba fedha za kujikimu wanazopewa wanafunzi wa vyuo vikuu maarufu kama 'Boom' ziondolewe na badala yake walipiwe karo moja kwa moja, kwani wanafunzi wengi wamekuwa na tabia mbaya ikiwemo kulewa kupitia fedha hizo.
.
CCM imesisitiza kuwa itaendelea kuisimamia Serikali ili kuongeza utoaji wa mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu wenye sifa stahiki, kama ambavyo imeahidi kwenye Ilani yake ya Uchaguzi (2020-2025) katika ukurasa wa 131.