Back to top

APC HOTEL & CONFERENCE CENTRE KUVUTIA WAWEKEZAJI

05 July 2024
Share

Katika kuunga mkono juhudi za Serikali ya Tanzania inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Uongozi wa kituo cha mikutano APC Hotel and Conference Centre wamejidhatiti kuhakikisha wanaweka mazingira wezeshi kwa wadau mbalimbali ili kuendelea kuvutia wawekezaji na watalii wengi nchini katika kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

Ameyasema hayo leo Julai 3, 2024 Jijini Dar es Salaam Afisa Mtendaji Mkuu wa kituo cha mikutano APC Hotel and Conference Centre Bw. Mkenganyi Wenceslaus wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya 48 ya biashara ya kimataifa SabaSaba huku akibainisha kuwa maonyesho hayo yameendelea kuwa fursa kwa wawekezaji na watu kutoka ndani na nje ya nchi kuja kujifunza na kutambua fursa mbalimbali za uwekezaji.

"Kiukweli maonyesho ya biashara ya kimataifa SabaSaba yameendelea kuwa chachu ya maendeleo kwetu katika kuhakikisha tunayatumia kuwafikia watu mbalimbali kwa kutambua sisi nini tunafanya ili waweze kuchangamkia fursa zitokanazo na APC, Hivyo tunaishukuru Serikali kwa kuendelea kuweka mazingira rafiki kwa watu kutoka sehemu mbalimbali duniani kuweza kuwekeza" amesema Wenceslaus 

Hivyo, Wenceslaus amesema wanajihusisha na kumbi za mikutano ambazo si chini ya 10 ambazo zinachukua kuanzia watu watano hadi elfu moja,  zinazohusisha mikutano ya ofisi na binafsi ambayo imeambatana na huduma za chakula pamoja na maladhi.