Back to top

"SUALA LA UTEKAJI KUMULIKWA KWA KINA"NKUBI

28 July 2024
Share

Wakati mchakato wa Uchaguzi wa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (Tanganyika Law Society - TLS), ukizidi kupamba moto, mmoja wa wagombea wa kiti hicho Wakili Sweetbert Nkuba, amesema endapo atashinda nafasi hiyo pamoja na mambo mengine atashauri itungwe sheria kali kwa watu ambao watakamatwa au wakaotapatikana na hatia kwenye masuala ya utekaji.

Ameeleza hayo kwenye mdahalo wa wagombea wa Urais wa TLS, uliofanyika kwenye ukumbi wa Wakili House Jijini Dar es Salaam, ambapo ameeleza kuwa suala la utekaji ni kama limekuwa sehemu ya uhalifu ambao umejichukulia nafasi kubwa.

"Nitakapokuwa Rais wa TLS Pamoja na baraza langu la uongozi sio tu utekaji lakini masuala yote ya uhalifu wa aina yoyote tutapigia kelele, mimi ni madau wa haki na ni mdau wa kupigania haki kwa hiyo kwenye suala la utekaji na uhalifu mwingine nakemea na kulaani kwa nguvu zote"Amesema Nkubi.

Aidha uchaguzi wa Rais wa TLS unatarajiwa kufanyika tarehe 3 Agosti 2024, katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.