Back to top

WAWILI WAKAMATWA KWA TUHUMA ZA MAUAJI MKOANI ARUSHA

09 October 2024
Share

Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limewakamata watuhumiwa wawili kwa tuhuma za mauaji ya Israel Paulo (36), Mkazi wa Leguruki, Wilaya ya Arumeru na Mkoa wa Arusha, aliyefariki dunia tarehe 05.10.2024 wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Tengeru baada ya kujeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili wake na watuhumiwa hao.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, SACP Justine Masejo amewataja watuhumiwa hao waliokamatwa kuwa ni Ndewario Lazaro maarufu kwa jina Shombotoni (60) Mkulima, Mkazi wa Mwaruvango Wilaya ya Arumeru na Oscar Ndewario (29) mkazi wa Moivaro ambaye alikamatwa huko Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara ambaye alitoroka baada ya tukio hilo.

Kamanda Masejo amesema upelelezi wa tukio hilo unaendelea na pindi utakapokamilika jalada litapelekwa ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa hatua zaidi za kisheria.

Jeshi la Polisi mkoani humo limewashukuru wananchi kwa namna ambavyo wanashirikiana katika kuzuia matukio ya uhalifu, na kuwaomba pia kufuata sheria na kuacha kujichukulia sheria mkononi.