Jumla ya ekari 3007.5 za mashamba ya bangi zimeteketezwa, huku jumla ya kilogramu 7,832.5, za bangi kavu na kilogramu 452 za mbegu za bangi zimekamatwa Pamoja na watuhumiwa 17 wamekamatwa na tayari wameshafikishwa mahakamani.
Hayo yamebainishwa na Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya DCEA Aretas Lyimo, wakati akitoa taarifa ya operesheni iliyodumu kwa muda wa wikitatu,
wilayani Tarime, mkoani Mara, iliyolenga kukabiliana na tatizo la uzalishaji na usambazaji wa dawa za kulevya hususan bangi.
Kwa upande wao wananchi wa Tarime wameridhia kuachana na kilimo cha bangi, mara baada ya operesheni hiyo.