Mwalimu Subiri Andson (37), wa shule ya sekondari Nguno wilayani Itilima mkoani Simiyu, anayetuhumiwa kwa kosa la kubaka mwananfunzi (17) ambaye jina lake limehifadhiwa amekutwa na kesi ya kujibu baada ya mahakama ya Wilaya ya Itilima kusikiliza mashahidi sita wa shauri hilo.
Hakimu Mfawidhi Mkazi wa Mahakama hiyo Robert Kaanwa, amesema Mahakama imemkuta Mtuhumiwa na kesi ya kujibu baada ya upande wa mashtaka ukiongozwa na mwendesha mashtaka Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Jaston Mhule, kutoa mashaidi sita wenye kielelezo kimoja.
Aidha, shauri hilo limeahirishwa hadi Oktoba 21,2024 na mtuhumiwa yupo nje kwa dhamana.
Inadaiwa kuwa mtuhumiwa aliwekwa chini ya ulinzi na wananchi baada ya kukamatwa akiwa na mwanafunzi chumbani kwake majira ya saa moja usiku.
Pia imeelezwa kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo oktoba 7,2024 katika kijiji cha Nguno wilayani ya Itilima mkoani Simiyu, katika maeneo ya shule hiyo ambacho ni kinyume na kifungu cha 130(1)(2)e na 131(1)cha sheria ya kanuni ya adhabu sura 16 kama ilivyofanyiwa marejeo ya mwaka 2022.