Back to top

JKCI YAFANYA UPASUAJI WA MOYO KWA NJIA YA ZOOM

20 October 2024
Share

Mgonjwa aliyekuwa akisumbuliwa na mishipa ya moyo na damu kuziba amefanyiwa upasuaji wa tundu dogo kwa njia ya mtandao na wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI),  kwa kushirikiana na wenzao kutoka nchi mbalimbali duniani. 

Akizungumza jijini Dar es Salaam mara baada ya kutoka kwenye chumba cha upasuaji wa moyo Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Dk. Khuzeima Khahbhai, amesema wamefanikiwa kubadilisha 'valve' za moyo na kuzibua mishipa ya damu iliyoziba kwa kushirikiana na wataalamu kutoka sehemu mbalimbali kwa njia ya mtandao (zoom meeting). 

“Tumefanya upasuaji wa kubadilisha valve za moyo na kuzibua mishipa ya damu bila kufungua kifua na mgonjwa yupo salama na sasa tunategemea baada ya siku mbili ataruhusiwa kwenda nyumbani” 

“Upasuaji huu unaitwa TAVr ambapo tulikuwa tukiufanya mubashara kupitia ZOOM kwa kujumuika na madatari wenzetu kutoka sehemu mbalimbali duniani kwa lengo la kubadilisha ujuzi na kujifunza jinsi upasuaji huu unavyofanyika,” amesema Dk. Khuzeima.