Back to top

MWIGULU NCHEMBA AMKOSOA MPINA BUNGENI, MPINA AOMBA RADHI

07 November 2024
Share

Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba, amemkosoa Mbunge wa Mhe. Kisesa, Luhaga Mpina kwa kulidanganya Bunge, jambo lililopelekea Mbunge huyo kuomba radhi na kufuta kauli zake.

Akitoa ufafanuzi juu ya jambo hilo Dkt.Nchemba amesema hakuna taasisi au kampuni binafsi yoyote inaruhusiwa kukusanya kodi na mapato yote yanakusanywa na TRA na TPA, toka Kampuni ya DP World kuanza shuguli zake ufanisi umeongezeka sana, makusanyo ya bandarini nayo yamepaa hadi Trilioni 1.23 kiwango ambacho hakijawahi kufikiwa toka TRA ianzishwe.

Baada ya ufafanuzi huo Dkt.Nchemba alimtaka Bunge huyo kufuta kauli zake za uongo na kuomba radhi na Mpina alikiri na kufanya hivyo.

Awali Mbunge huyo alitoa Kauli ambayo haikua ya kweli Bungeni kwa kusema Kampuni ya DP World inakusanya kodi bandarini.

Naibu Spika Mhe Zungu ametumia fursa hiyo kumpongeza Waziri wa Fedha kwa kutoa ufafanuzi mzuri unaoeleweka na kuwataka Mawaziri wengine kuiga mfano wake ili kudhibiti upotoshaji ndani ya Bunge.