Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Hassani Mwamweta amesema serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imejidhatiti katika kujenga mazingira rafiki kwenye Sekta ya Utalii ili kukuza utalii wa Tanzania, kuvutia uwekezaji na kukuza Soko la Utalii.
Balozi Mwamweta ametumia fursa hiyo kueleza kuwa Mamlaka za Tanzania zitaendelea kutoa huduma bora kwa watalii wote wanaotembelea hifadhi za Tanzania, ikiwezo huduma ya 'Visa on arrival'.
Balozi Mwamweta ameyasema hayo wakati akifungua Maonesho ya Utalii ya 'My Tanzania Roadshow 2024' Jijini Frankfurt, Ujerumani yaliyoratibiwa na kampuni ya utalii ya KiliFair kwa kushirikina na Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) pamoja na Hifadhi ya Ngorongoro.
Balozi Mwamweta ameyaeleza makampunu makubwa ya Utalii nchini Ujerumani kuwa hayatajutia kuifanya Tanzania kama chaguo namba moja la kupeleka watalii pamoja na kuwekeza kwenye utalii