Back to top

SAKATA LA UMRI MITANDAONI LAPAMBA MOTO AUSTRALIA

21 November 2024
Share

Serikali ya Australia imetishia kutoza faini ya mamilioni ya dola kwa kampuni za mitandao ya kijamii, zitakazokiuka pendekezo la kupiga marufuku watoto walio chini ya miaka 16 kutumia huduma zao.

Waziri wa Mawasiliano Michelle Rowland, aliwasilisha marekebisho ya Sheria ya Usalama Mtandaoni bungeni siku ya Alhamisi, ambayo serikali imeyataja kama "mageuzi yanayoongoza duniani kwa mitandao ya kijamii."


Sheria hiyo inajumuisha adhabu za kifedha za hadi dola milioni 50 za Australia (dola milioni 32.5) kwa kampuni ambazo hazijachukua "hatua zinazofaa kuzuia watumiaji walio na vizuizi vya umri kuwa na akaunti.

Marufuku hiyo inatarajiwa kutumika kwa huduma za mitandao ya kijamii zikiwemo TikTok, X, Instagram na Snapchat, ingawa orodha ya huduma zilizopigwa marufuku haijatolewa.