Back to top

Asilimia 40 ya wanaume wenye UKIMWI ndo hutumia dawa za kufubaza.

28 May 2018
Share

Utafiti uliofanywa na Tume ya Taifa ya kudhibiti UKIMWI TACAIDS umeonyesha asilimia  40  tu ya wanaume wanaogundulika kuugua maradhi hayo ndio wanafanya vipimo na kutumia dawa za kufubaza makali ya ugonjwa huo hali inayochangia idadi ya vifo kuongezeka katika kundi hilo.

Takwimu hizo zinatolewa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS Jumanne Isango katika mkutano wa kuzijengea uwezo konga za waishio na virusi vya ukimwi kuhusu sheria ya ukimwi ambapo anasema tafiti  zinaonyesha wanaume wanaongoza kwa idadi ya vifo kutokana na kuchelea kutumia dawa za kufubaza makali ya ugonjwa huo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa ufuatiliaji na tathmini kutoka TACAIDS Dk Jerome Kamwela anasema asilimia 52 tu ya Watanzania wanaoishi na virusi vya ukimwi ndio wanajua hali zao ambapo kati yao asilimia 90 wanatumia dawa za kufubaza virusi .

Cosmas Kurwa ni Hakimu kutoka Dodoma anahoji kuhusu matumizi ya misaada inayotolewa na mataifa wahisani katika vita ya ungonjwa huo kuwa vina masharti kwenye matumizi yake huku Rose Kosuri ambaye ni muathirika wa maradhi hayo akitaka kujua uhalali wa taarifa za watu wanaofanya vipimo binafsi vya ugonjwa huo.