Back to top

Mkutano wa viongozi wa marekani na Korea Kaskazini waanza

11 June 2018
Share

Mkutano wa mwisho wa matayarisho ya mkutano wa kihistoria wa Viongozi wakuu wanchi za marekani na Korea Kaskazini unaendelea nchni Singapore.

Mkutano huo wa matayarisho ulianza saa nne asubuhi ya leo kwa saa za Singapore ambapo balozi wa Marekani nchini Ufilipino SUNG KIM anashiriki.

Balozi huyo amekuwa akiongoza majadiliano ya Marekani na Korea Kaskazini.

Kiongozi Mkuu wa Korea Kaskazini Kim Jong Un aliwasili Singapore majira ya saa nane na nusu mchana jana Jumapili na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu LEE HSIEN LOONG wa Singapore.

Huku Rais DONALD TRUMP wa Marekani pia aliwasili kwenye uwanja wa ndege wa jeshi nchini Singapore takribani saa mbili na nusu usiku jana hiyo hiyo kwa saa za eneo hilo na kufikia katika hoteli iliyo katikati ya jiji.

Suala muhimu kwenye mkutano huo wa viongozi wakuu unaofanyika kesho jumanne litakuwa ni kwa kiwango gani Rais DONALD TRUMP na KIM JONG UN wataweza kuandaa mpango thabiti wa Korea Kaskazini kuachana na silaha za nyuklia.