Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.John Pombe Magufuli amemteua Jaji Mstaafu Damian Zefrin Lubuva kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi huo umeanza leo tarehe 18 Juni, 2018.
Jaji Mstaafu Lubuva anachukua nafasi ya aliyekuwa mwenyekiti wa baraza hilo Bw. Peter Ngumbullu.