Back to top

Viazi lishe kinga ya afya ya macho.

27 June 2018
Share

Serikali imezindua mpango maalum wa kilimo cha viazi lishe katika shule za msingi na sekondari ili kutatua tatizo la ukosefu wa chakula mashuleni baada viazi hivyo kubainika kuwa na uwezo wa kuongeza kinga ya mwili kwa watumiaji wake hatua ambayo pia itawezesha wanafunzi kuepukana na tatizo la afya ya macho na hivyo kuipunguzia serikali gharama ya kusambaza kila wakati kinga ya matone ya vitamini "A".

Akizungumza wakati wa kuzindua mpango huo wa kilimo cha viazi lishe kupitia mbegu ya zilizoboreshwa na kituo cha utafiti wa kilimo cha ukiruguru za kabode na mazao katika wilaya ya Butiama mkoani Mara, Mratibu wa Kanda wa kituo hicho Bw.Simon Jeremia, amesema zao hilo sasa litapandwa katika ngazi ya familia kwa kuhusisha shule zote za msingi na sekondari.

Naye afisa kilimo wa mkoa wa mara Bw. Denis Nyakisinda, akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango huo kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Mara, ameagiza maafisa kilimo ngazi ya kata kuchukua hatua za kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika kilimo cha zao hilo la viazi lishe na kusema mkoa umeanza taratibu za ujenzi wa kiwanda cha kusindika zao hilo katika kuliongeza thamani.