Wananchi wa kijiji cha Lilondo halmashauri ya wilaya ya Madaba wilayani Songea mkoani Ruvuma wamejitokeza kwa wingi kuchimba Mitaro na kufukia mabomba katika mradi wa maji wa Lilondo utakaogharimu shilingi milioni 6o hadi kukamilika ili kutatua tatizo la maji katika kijiji chao.
Wananchi hao wanasema kuwa wameamua kuchukua hatua badala ya kuisubiri serikali kwa kila kitu na kuona katika kijiji chao kuna shida kubwa ya maji ambapo hadi sasa wametumia shilingi milioni 20 katika mradi huo.
Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Madaba Mheshimiwa Joseph Mhagama amechangia shilingi milioni tano na mabomba ili kutatua tatizo la maji katika kijiji cha Lilondo.
Naye mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Madaba Bw. Vastus Mfikwa amemshukuru mbunge Joseph Mhagama kwa kushiriki katika kuchimba mtaro na kutandaza mabomba katika mradi huo.