Waziri wa nishati Dkt. Medard Kalemani ameiagiza mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji EWURA na bodi ya shirika la umeme TANESCO kukaa pamoja na kutafuta mbinu za kupunguza bei za upatikanaji wa huduma ya umeme ili kuwapunguzia wananchi gharama za matumizi ya nishati hiyo muhimu kwa ukuaji wa uchumi
Akizungumza katika kikao kazi kilichohusisha watendaji wa wizara ya nishati wakala wa usambazaji umeme vijijini REA pamoja na mameneja wa mikoa na kanda wa shirika la umeme nchini TANESCO waziri Dkt. Kalemani amesema wananchi wanahitaji huduma ya nishati na kuwataka watendaji hao kuona namna ya kumpunguzia mwananchi aweze kumudu gharama za upatikanaji wa huduma hiyo.
Aidha katika hatua nyingine waziri Dkt. Kalemani ameiagiza bodi ya shirika la umeme nchini TANESCO kuwachukulia hatua mameneja wa mikoa na kanda watakaoshindwa kuwaunganishia wananchi umeme kwa wakati.
Kwa upande wake kaimu mkuugenzi mkuu wa EWURA Bw. Nzinyangwe Mchany amesema bodi ya mamlaka hiyo ipo kwenye mchakato wa kukaa pamoja ili kuzipitia upya gharamna za upatikanaji na uendeshaji wa huduma za nishati ya umeme kwa wananchi nchi nzima.