Mkuu wa wilaya ya Tabora mjini Bw.Komanya Erick amemwagiza mkurugenzi wa Manispaa ya Tabora kuwaondoa kazini na wakuu wa idara ambao wamekuwa ni changamoto kwa jamii na kusababisha migogoro, hususani idara za mipango miji na ardhi, kwa lengo la kuijenga manispaa ambayo ina hati yenye mashaka.
Bw. Komanya Eriki amesema kuwa, malalamiko na changamoto zinazowakabiri wananchi zimekuwa zikisababishwa na wakuu wa idara ambao hawataki kuwajibika na kujifanya miungu watu katika kutekeleza majukumu yao na hivyo suluhisho ni kuwaondoa nafasi zao wapewe watendaji ambao watakubali kuwajibika.
Baadhi ya madiwaniwamedai kuwa, watumishi kukaa katika kutuo kimoja kwa muda mrefu kumekuwa kukisababisha watendaji kufanyakazi kwa mazoea na kuwaona wananchi kama hawahitaji huduma, na hivyo rai ya mkuu wa wilaya ni wakati muafaka kuwahamisha watendaji katika vitengo.