Back to top

Kiwanda cha Sukari Kagera chaelemewa na mrundikano wa Sukari.

03 September 2018
Share

Kiwanda cha Sukari Kagera kimejikuta katika wakati mgumu kutokana na kukithiri kwa mrundikano wa shehena ya sukari inayozalishwa kiwandani hapo kutokana na kukosa wanunuzi na kujikuta wakitafuta maeneo ya nje ya kiwanda hicho ili kuifadhi Sukari hiyo jambo ambalo limekuwa likiwapa changamoto katika shughuli za uzalishaji.

Hayo yamejiri mkoani Kagera  wilaya ya Misenyi ambapo uongozi wa kiwanda hicho umesema hali hiyo si yakawaida katika uzalishaji wao wa sukari kwani kwa sasa maeneo yaliopo  ndani ya kiwanda hicho yamejaa na sasa kilichobaki ni kuandaa maeneo ya nje ili kuhifadhi sukari hiyo huku mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa kiwanda hicho Bwana Seif Seif akielezea sababu ya mrundikano huo.

Kutokana na kiwanda hicho kutoa ajira kwa wafanyakazi wa ndani na wa nje wafikao 42000 naibu waziri mwenye dhamana ya kazi vijana na ajira Mhe. Anthony Mavunde  amepokea kilio cha wafanyakazi wa kiwanda hicho wakati alipofanya  ziara yake katika kiwanda hicho mkoani Kagera baada ya hofu juu ya hatnma ya ajira zao iwapo hali hiyo itaendelea.