Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Korogwe Mhe. Hilary Ngonyani amesema mkuu wa idara ambae atakua hajavaa suti kwenye vikao vyovyote vinavyofanyika vya halmashauri ya mji wa Korogwe atatolewa nje ya ukumbi.
Ametoa agizo hilo akiwa kwenye kikao cha pamoja kati ya watumishi hao pamoja na madiwani wa halmashauri hiyo huku akiwataka wakuu hao wa idara kuiga mfano wa madiwani ambao huonekana nadhifu.
Pamoja na watumishi hao kutakiwa kuwa nadhifu lakini halmashauri hii imeweza kufanya vizuri kwenye matokeo ya mtihani wa darasa la saba kimkoa na kitaifa na hiyo ni baada ya kushika nafasi ya thelasini na tatu kitaifa huku kimkoa ikishika nafasi ya pili.