Back to top

Waziri Mkuu aridhishwa na mradi wa ujenzi wa viwanda 11 Tanga.

31 October 2018
Share


Waziri Mkuu Mh.Kassim Majaliwa ametembelea eneo la mradi wa ujenzi wa viwanda 11 katika kijiji cha Mtimbwani wilaya ya Mkinga mkoani Tanga, ambapo amesema ameridhishwa na hatua za awali za uwekezaji huo.

Amesema uwekezaji huo unatarajiwa kulinufaisha taifa na wananchi wakazi wa wilaya ya Mkinga kwa kuwa kinatarajiwa kuajiri zaidi ya watu 8,000, hivyo amewaomba wananchi hao waendelea kutoa ushirikiano kwa wawekezaji hao.