Back to top

Jeshi la polisi latoa tahadhari mauaji ya watoto Njombe.

17 January 2019
Share

Jeshi la polisi mkoani Njombe limewataka wananchi kuchukua tahadhari za watoto wa dogo kufuatia ongezeko la matukio ya utekaji wa watoto  wilayani Njombe ambapo kwa kipindi cha mwezi Desemba 2018 mpaka Januari 17 2019 watoto wanne wameripotiwa kutekwa na wawili kukutwa wakiwa wamefariki na miili yao kutupwa katika misitu na wengine kuokolewa wakiwa wamejeruhiwa.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Njombe kamishina msaidizi Rashid Ngonyani ametolea ufafanuzi matukio ya utekaji wa watoto ambapo amesema badhi ya watoto waliotekwa wamenusurika vifo huku baadhi wakikutwa wameuawa ambapo hata hivyo amekanusha uvumi uliopo kuwa baadhi ya miili kukutwa ikiwa imeondondolewa viungo zikiwemo sehemu za siri.