Back to top

Mvua ya mawe yaharibu mashamba na kubomoa majengo ya shule Kigoma.

22 March 2019
Share

Mvua kubwa ya mawe iliyoambatana na upepo imeharibu zaidi ya ekari 100 za shamba la mbegu la wakala wa mbegu za kilimo nchini lililopo katika kijiji cha Bugaga wilayani Kasulu mkoani Kigoma huku ikuezua paa za nyumba kadhaa na kubomoa kuta za majengo ya vyumba 4 vya madarasa katika shule za msingi Nyaruhande na Bugaga zilizopo wilayani humo .

ITV imefika katika maeneo ya shamba hilo la wakala wa mbegu za kilimo na kushuhudia uharibifu uliotokana na athari za mvua ambapo mtaalamu wa mbegu kutoka wakala huo Baraka Mbenye akisema uharibufu  ni kubwa.

Kamanda wa polisi mkoa Kigoma Martin Ottieno ameema jitihada za kuwasaidia watu walioathirika na mvua hizo zinaendelea.