Back to top

Kifusi machimbo ya madini chaua 1 Mwanza, 8 waokolewa, 1 anatafutwa.

10 September 2019
Share

Mtu mmoja amefariki dunia, mmoja akiwa hajaokolewa na wengine wanane wakiokolewa wakiwa hai baada ya kufukiwa na kifusi katika machimbo ya madini wilayani misungwi mkoani Mwanza.

Kamanda wa polisi mkoa wa mwanza ACP Mulilo Jumanne Mulilo amesema wanaendelea kufatilia chanzo cha tukio hilo ingawa taarifa za awali zinaonyesha limechangiwa na kudondoka kwa gema katika shimo hilo ambapo jitihada za kumpata mchimbaji mmoja ambaye ajapatikana zinaendelea.