Back to top

Serikali yaanza kutumia Oil chafu na pilipili kudhibiti Tembo

28 November 2019
Share

Wizara ya maliasili na utalii kwa kushirikiana na serikali ya wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, imeanza mkakati wa kutengeneza uzio wa oil chafu  na pilipili elfu moja kwa vijiji 10 ambavyo vimeathirika zaidi na Tembo wanaoharibu mazao na pia kuua watu.

Afisa wanyamapori mkuu kutoka wizara ya maliasili na utalii, Bw.Faustine Masaru amewahakikishia wananchi wa Tunduru kudhibiti Tembo huku akisema kuwa ongezeko la Tembo hao linatokana na  kuwadhibitiwa kwa majangili.