Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania TCAA imefuta kibali kilichokuwa kikiruhusu ndege za Shirika la ndege la Kenya kutua Tanzania.
Akizungumza na katika mahojiano maalum Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Hamza Johari amesema uamuzi huo umekuja baada Kenya kutoijumuisha Tanzania katika orodha ya nchi ambazo raia wake wataruhusiwa kuingia Kenya.
Kwa upande wake Waziri wa Uchukuzi nchini Kenya James Macharia amesema kuwa wamepokea taarifa hiyo kutoka Serikali ya Tanzania huku akikanusha taarifa ya ndege za Tanzania kuzuiwa kuingia nchini Kenya na kueleza kuwa waliamua ndenge za Tanzania zinapoingia Kenya abiria wake wangetakiwa kukaa karantini ndani ya siku 14.
Naye Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano nchini Tanzania mhandisi Isack Kamwele amesema kutakuwa na kikao siku ya Jumanne kilichoitishwa na Wizara ya Mambo ya Nje ili kujadili suala hilo.