Back to top

NCCR Mageuzi ikiingia madarakani kuanza na katiba mpya.

05 September 2020
Share

Mgombea Urais wa chama cha NCCR-Mageuzi Bwana Yeremia Maganja amesema akishinda nafasi hiyo ndani ya miezi kumi na miwili hadi kumi na minane katiba mpya itapatikana ambayo itakuwa mwanzo wa mwafaka wa kitaifa.

Ametoa ahadi hiyo alipowahutubia wananchi katika uzinduzi wa kampeni ya chama hicho jijini Dar es Salaam.

Naye mgombea mwenza Bwana Haji Ambari Khamis amesema anataka kuona uchaguzi hasa kule Zanzibar unakwenda salama, hivyo wanaohuska wahakikishe hilo linafanyika.

Kabla ya kumkaribisha mgombe Urais wa chama hicho, Mwenyekiti wa Taifa wa NCCR Mageuzi Mhe.James Mbatia amesema taifa linapaswa kushikamana na siyo watu kuishi kwa hofu.

Katibu Mkuu wa chama hicho Elizabeth Mhagama amesema ilani ya NCCR Mageuzi iliyozinduliwa leo imepwa jina la Ilani ya Mwafaka wa Kitaifa.