Back to top

Mbegu feki za ufuta zawatesa wakulima wa Lindi na Mtwara.

15 January 2021
Share

Ukaguzi wa mbegu uliyofanywa na taasisi  ya kudhibiti ubora wa mbegu  nchini TOSCK katika mikoa ya lindi na mtwara umebaini uwepo wa mbegu feki za ufuta katika baadhi ya maduka yanayouza mbegu hizo,  hali inayowakatisha tamaa  wakulima wa zao hilo kuandaa mashamba  hasa kipindi hiki cha  upandaji wa  zao hilo.
.
Akizungumza mara baada  kufanya ukaguzi  wa mbegu katika maduka yanayouza  mbegu  mbalimbali ikiwemo ya ufuta na mahindi mkaguzi wa mbegu kanda ya kusini Bw. Diksoni Rwabulalala amesema wapo baadhi ya wafanyabishara  wamekuwa wakiuza mbegu feki hali wakijua kufanya hivyo ni kosa.
.
Amesema katika ukaguzi uliyofanyika katika mkoa wa lindi na mtwara yapo baadhi ya maduka yamebainika kuuza mbegu feki na baadhi yao kufungiwa kufanya biashara hiyo.
.
Amesema  uuzaji wa mbegu feki za ufuta umechangia baadhi ya wakulima kugoma kuendelea kulima zao hilo kutokana na kupata hasara kila mwaka pia ametumia fursa hiyo kuwaonya  wafanyabiashara wanaouza  mbegu kununua bidhaa hiyo kwenye makampuni pasipo kupewa risiti jambo ambalo amesema ni kosa kisheria.
.
Hata hivyo amesema taasisi hiyo itaendelea kutoa elimu kwa wauza maduka ya mbegu  ili  wauze mbegu  zenye ubora na zilizothibitishwa na taasisi hiyo.
.
Kwa upande wao wauzaji  wa  maduka ya mbegu wameomba elimu iendelee kutolewa kwani wakati mwingine makampuni ya mbegu yanawauzia mbegu zisizofaa na hivyo kuangukia kwenye mkono wa sheria.