Back to top

Bangi tishio kwa wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari Arusha.

23 January 2021
Share

Matumizi ya dawa za kulevya ikiwemo bangi yameendelea kushika kasi mkoani Arusha huku yakiwaathiri zaidi vijana baadhi yao wakiwa  bado wanasoma shule za Msingi na Sekondari.

Kauli hiyo imetolewa na wadau wanaosaidia vijana akiwemo Mratibu wa afya ya akili mkoa wa Arusha Bw. Charles Migunga walipokutana na  waandishi wa habari kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kusaidia kudhibiti tatizo hilo ambalo amesema jitihada za ziada za kukabiliana na tatizo hilo zinahitajika.

Kwa upande wao baadhi ya wazazi na wadau wanaosaidia vijana wamesema upo uwezekano wa kudhibiti tatizo hilo kama kila idara na kila  mmoja atatimiza wajibu wake.

Licha ya kuwepo kwa jitihada kubwa za kubabiliana na tatizo la dawa za kulevya nchini, hali bado sio shwari kwani wakati Arusha  ikitajwa kuwa miongoni mwa mikoa inayostawisha zao la bangi Tanzania pia inatajwa kuwa miongoni mwa nchi za ukanda wa Afrika  Mashariki zenye idadi kubwa ya watumiaji wa dawa za kulevya.