Back to top

Mizinga ya nyuki mia mbili yagaiwa kwa wananchi Gairo.

13 March 2021
Share

Katika kuinusuru wilaya ya Gairo kugeuka jengwa kutokana na mabadiliko ya tabia nchi pamoja na uharibifu wa mazira unaofanywa na wananchi kwa kufyeka misitu  kiholela,wakala ya wa huduma za misitu nchini TFS imetoa mizinga 200 ya nyuki kwa wakazi wa vijiji 10 vya wilaya ya Gairo ili  waondokane na shughuli zinazopelekea uharibu wa mazingira.

Akikabidhi mizinga hiyo kwa mkuu wa wilaya ya Gairo kwa ajili ya kuwagawia wafugaji wa nyuki wilayani humo kamishna msaidizi usimamizi wa rasilimali za nyuki TFS Hussein Msuya amesema utafiti unaonesha wilaya ya Gairo kuwa na asali nzuri inayozalishwa kutokana na aina ya miti inayopatikana katika maeneo hayo.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Gairo BI.Siriel Nchembe serikali itaendelea kuwasaidia wazalishaji na wasindikaji wa asali ili zao hilo liwanufaishe katika uendelezaji wa familia zao huku akikemea tabia ya baadhi ya wananchi wasio waadilifu kuchoma miti ovyo hatua inayosababisha uharibifu wa uoto wa asili katika wilaya hiyo.

Nao baadhi ya wanachi waliopokea mizinga hiyo wameishukuru TFS kuwapatia mizinga hiyo na kuahidi kuitunza vizuri ili iweze kuwanufaisha na kukuza uchumi wao na taifa kwa ujumla.