Back to top

Safari za Treni ya Mwendokasi SGR kuanza Augosti mwaka huu.

13 March 2021
Share

Safari za reli hiyo zinatarajiwa kuanza Agosti mwaka huu katika kipande cha Dar es Salaam - Morogoro.

Kamati ya kudumu ya bunge ya miundombinu imekagua mradi wa Treni ya mwendokasi SGR kutoka Dodoma hadi Dar es Salaam ambapo Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Leonard Chamuriho amesema safari za reli hiyo zinatarajiwa kuanza Agosti mwaka huu katika kipande cha Dar es Salaam - Morogoro baada ya vichwa na mabehewa ya treni kuwasili Juni 2021.

Wakikongea na ITV wakati wa ziara ya kamati hiyo ikikagua mradi huo kutoka Dodoma hadi Dar es Salaam baadhi ya wajumbe wa kamati wamesema mradi huo utaleta manufaa makubwa endapo wananchi watautumia baada ya kukamilika.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya miundombinu Mhe. Selemani Kakoso amesema wameridhishwa na ujenzi wa mradi huo huku akisisitiza kulipwa fidia kwa wananchi ambao reli hiyo inapita.

Akizungumza baada ya wajumbe wa kamati hiyo kutembelea mradi huo Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Leonard Chamriho amesema baada ya vichwa na mabahewa ya treni kuwasili, Julai watafanya majaribio ya safari.