Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro imewazuia kuendelea na safari ngamia 89 waliokuwa wakisafirishwa kwa miguu kutoka Kenya kwenda Dar es salaam wakiongozwa na raia watatu wenye asili ya Somalia ambao hati zao za kusafiria na usafirishaji wa wanyama hao zina utata mkubwa.
Mkuu wa wilaya hiyo Bw Abdallah Mwaipaya ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati hiyo amesema, hatua hiyo imechukuliwa ili kuchunguza uhalali wa hati hizo.