Back to top

Mikoa ya Pwani na Dar es Salaam yatajwa kuongoza migogoro ya Ardhi.

14 July 2021
Share

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.William Lukuvi amesema mikoa ya Pwani na Dar es Salaam ndiyo inayoongoza kwa uvamizi wa ardhi za watu kwa kutumia nguvu kinyume na utaratibu.

Mhe.Lukuvi amesema hayo wakati wa uzinduzi wa kampeni maalumu ya kusikiliza, kutatua na kutokomeza migogoro ya ardhi katika mkoa wa Pwani uluohudhuriwa na wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa huo.

Amesema mkoa wa Pwani ni eneo muhimu kwa uwekezaji kwa hiyo haiwezekani kuwaachia watu kuvamia maeneo ya viwanda, mashamba, maeneo ya  umma na maeneo ya wazi ambayo yapo kisheria.

Amemtaka kila mkuu wa wilaya aitambue migogoro ya ardhi katika maeneo yake, awe na taarifa ya kina ya kila mgogoro na atengeneze daftari la  migogoro ya ardhi kwa kushirikiana na wataalam wa ardhi katika kuitatua na kama kuna ofisa ardhi siyo muadilifu apelekwe kwake ili amchukulie hatua.