Waziri wa Nishati Dkt.Medard Kalemani ameagiza kusimamishwa kazi watumishi watatu wa Shirika la Umeme Tanzania ili kupisha uchunguzi baada ya kituo cha Kupokea, Kupooza na kusambaza umeme kilichopo Msamvu Manispaa ya Morogoro kuteketea kwa moto akieleza kuwepo kwa viashiria vya uzembe.
Waziri Kalemani ametoa agizo hilo baada ya kutembelea katika chanzo cha moto huo kilichopo eneo la ujenzi wa reli ya SGR nakubaini kuwepo kwa uzembe.
Waziri Kalemani amelitaka Shirika la Umeme nchini mkoa wa Morogoro kuhakikisha umeme unarudi ndani ya saa 24 kwa maeneo ambayo hayana umeme.
Mkuu wa Mkoa wa Morogro, Bw.Marten Shigela amewashukuru wafanyakazi wa shirika la umeme kurejesha haraka umeme katika baadhi ya maeneo.