
Serikali wilaya ya Muleba mkoani Kagera imewakamata vijana watatu wakazi wa wilaya hiyo kwa tuhuma za kujihusisha na usafirishaji wa samaki aina ya Sangara kilo mia nne zenye thamani ya shilingi milioni nne zilizokuwa zikitoka mwalo wa Ruhanga kata ya Magata kuelekea wilayani Karagwe zilizovuliwa kinyume na sheria ya uvuvi.
Mkuu wa wilaya ya Muleba Toba Nguvila akiwa katika eneo la tukio amewataka wananchi kujiepusha kujihusisha na mtandao wa uvuvi haramu kwa kuwa tayari serikali imeunda kikosi kazi kwa ajili ya kupambana uvuvi usiozingatia sheria ili kuendelea kulinda rasilimali za Ziwa Victoria na ziwa Buringi.