Back to top

Jaji Tiganga kuendelea na kesi ya Mbowe na wenzake.

26 October 2021
Share

Kesi inayokabili  Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe na wenzake yapata Jaji Mpya ambaye ni Jaji Joachim Tiganga ambaye anaendelea kusikiliza kesi hiyo na kwa sasa shahidi upande wa Jamhuri ACP Ramadhani Kingai Kamanda wa Polisi Kinondoni anaendelea kutoa ushahidi wake.

Jaji Tiganga amejitambulisha mahakamani hapo mbele ya washtakiwa na upande wa mashtaka.

Jaji huyo anachukua nafasi hiyo baada ya Jaji Mustapha Siyani, kujiiondoka katika shauri hilo kutokana na kile alichodai kuwa amekuwa na majukumu mengine baada ya Kuteuliwa kuwa Jaji Kiongozi.